Friday, August 14, 2009

USINYWE RED BULL -- NI HATARI KWA MAISHA YAKO – HASA VIJANA


RED BULL Huuzwa  katika maduka makubwa (Supermarkets) na madogo (Retail
Shops) katika nchi ya Tanzania na watu wazima na watoto wetu wengi wana
mazoea ya kunywa kinywaji hiki ambacho kinaweza kusababisha kifo!

Kemikali zinazopatikana katika kinywaji cha RED BULL zilitengenezwa maalum
katika maabara za kijeshi za Ma rekani kwa ajili ya kutuliza mzuka wa
maaskari wao wakati wakitekeleza mauaji ya kikatili sana dhidi ya
wananchi wa Vietnam miaka ya sitini na sabini. Kemikali hizo zilitumika
pia kama dawa ya kuwazindua watu waliozirai (“stress coma”).
Hazikukusudiwa kutumiwa kama kinywaji au kilevi cha kawaida!

Duniani kinywaji hiki (RED BULL) huuzwa kama kitu cha kuleta msismko
(Energizer Drink) na matangazo yake yanataja sifa zake kama ifwatavyo.

“Ni kinywaji kinachompa mtu nguvu ya kustahimili na umakini. Humpa mtu
kasi ya vitendo” ... na kadhalika.

RED BULL imesambaa katika nchi 100 kwa mpigo (nchi masikini!). Na
matangazo yake kuwalenga vijana na watoto, hasa wanamichezo. Hawa ni
rahisi kushabikia kinywaji hiki kibaya na kudhurika kiafya baadaye.

Katika hali yake ya matumizi ya sasa kinywaji hiki kiligunduliwa na
Mjerumani Dietrich Mateschitz ambaye alikikuta huko Hong Kong kikiwa ni
mojawapo ya madawa yaliyotumika katika kutengeneza dawa ya mswaki wa
meno.

Dawa hiyo ilitengenezwa kwa kemikali ambazo zina kafeni na taurini
(“caffeine and “taurine). Mjerumani huyo aliona vijana wajinga wa huko
wakishabikia unywaji wake akaona mwanya wa kufanya biashara na akafanikiwa
kukileta ulaya.

ATHARI ZA KUNYWA RED BULL

Kinywaji kinachotengenezwa na kusambazwa leo hivi kina kemikali mbaya
iitwayo “Glucuronolactone”, kemikali hatari ambayo ilitengenezwa na idara
ya jeshi la Marekani wakati wa vita na Vietnam kwa ajili ya kutuliza
mvurugiko wa mwazo wa maaskari wake uliotokana na mauaji ya kinyama
waliokuwa wanafanya huko Vietnam.

Kwa sababu ya madhara makubwa ya kinywaji hiki nchi za FRANCE na DENMARK
zimepiga marufuku kinywaji hiki na kibatiza jina la “MKOROGO WA UMAUTI”.
Katika nchi hizi, utafiti uligundua kuwa maaskari wa Marekani waliotumia
kinywaji chenye kemikali ya “GLUCURONOLACTONE” waliishia kupata madhara ya
maumivu makali ya kichwa, uvimbe wa ubongo na hata ugonjwa wa ini
(Migraines, Cerebral tumours and liver diseases). Ni kwa sababu hiyo
wamarekani waliacha kuwapa maaskari wao hicho kinywaji katika miaka ya
sitini na sabini.

Jambo la kushangaza ni kuwa lebo ya RED BULL inaonyesha wazi kuwa kinwaji
hiki kimetengenezwa kwa kemikali hatari ya “GLUCURONOLACTONE”! Ni kwa
sababu hiyo serikali za Denmark na Ufaransa nazo zikapiga marufuku unywaji
wa RED BULL.

Pamoja na wauzaji wa RED BULL kuweka bayana kuwa ndani mwake mna hiyo
kemikali hatari ya “GLUCURONOLACTONE” lebo ya RED BULL hailezi madhara
makubwa yanayoletwa na kemikali hiyo. Madhara ambayo hayakuwekwa bayana
kwa mnywaji ni kama yafuatayo:

1.Ni hatari kwa mtu ambaye hafanyi kazi au mazoezi mazito sana kukitumia
kwani kina tabia ya kuongeza msukumo wa damu na kasi ya mapigo ya moyo
kiasi kwamba mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa moyo.
2.Mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa damu kuvuja ubongoni kwani RED
BULL ina kemikali zinazoifanya damu iwe nyembaba ili moyo upate kusukuma
damu nyingi bila kutumia nguvu nyingi.
3.Ni hatari kuchanganya RED BULL na pombe ya aina yoyote kwani
mchanganyiko wake huwa ni sumu (“Deadly Bomb”) inayoathiri musuli za ini
la mtumiaji na kuiacha katika hali ambayo haitapona kamwe.
4.RED BULL Ina vitamini B12 kwa wingi, vitamini ambayo hutumiwa kama dawa
ya kuwazindua wagonjwa mahututi. Matumizi ya vitamini hii katika watu
wazima ina athari za kuleta shinikizo la damu na humfanya mtu ajisikie
kama mlevi.
5.Unywaji wa RED BULL mara kwa mara huvuruga mfumo ya neva za fahamu na
husababisha maradhi mithili ya mfadhaiko wa akili usioponyeka.

HITIMISHO::
RED BULL ni kinywaji HATARI SANA ambacho hapana budi kipigwe marufuku
katika nchi zote zinazoendelea kwani ni dhahiri kimetengenezwa na
kusambazwa ili kiathiri afya za wananchi wasiojiweza wa nchi hizi
masikini. Kwa kuwa wengi katika nchi hizi hutumia pombe za kila aina ni
wazi kuwa kinywaji hiki kinalenga kuwamaliza watu wetu – kana kwamba
ukimwi uliobuniwa na hao wabaya wetu hautoshi! N I VYEMA TUKAWALINDA
WATOTO NA VIJANA WETU LA SIVYO HATUNA WARITHI!

Tafsiri – EGM 2009

1 comment:

  1. Yeaaaaaah man, nimekubali kweli bab'lon system u"cpime, Big up sana mwanaharakat kwa ku2update manake tutaangamia mseiya. Endeleza mchakato Ras. Mo fire. C'lazima"

    ReplyDelete