Friday, August 7, 2009

Marekani Kutoa Msaada Wa Kijeshi Kwa Somalia


Marekani imeahidi Kuendelea kutoa msaada wa kijeshi kwa Somalia ili kuisaidia ili kuweza kuisadia serekali kupambana na wapiganaji wa kiislam.Akitoa ahadi kwa rais wa Somalia yaliyofanyika jana jijini Nairobi waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton alisema rais Obama na serikali yake wako tayari kutoa misaada mbalimbali serekali hiyo kufikia malengo yake ya kuingoza nchi nzima.Nchi ya Somalia kwa karibu miongo miwili sasa imekosa serekali imara baada ya kuibuka makundi mbalimbali ya kivita yakipambana huku kila kundi likitaka kuongoza nchi lakini kwa hivi sasa kundi kubwa la Kiislam la al-Shabab ndilo linaloonekana kuwa na nguvu zaidi baada ya kuwa limeshikilia sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia.

No comments:

Post a Comment