Friday, August 7, 2009

PAKISTAN


Maafisa usalama wa Marekani pamoja na Pakistan wamesema huenda kiongozi wa Taliban nchini Pakistan ambaye alikuwa akiongoza mashambulizi ya kujitoa mhanga dhidi ya serikali ya Pakistan Chief Baitullah Mehsud ameuawa ktk mashambulizi ya roketi yaliyofanywa na kikosi cha CIA.Habari zinazidi kusema kwamba katika mashambulizi hayo yaliyofanywa na CIA dhidi ya vikosi vya Taliban huenda Mehsud ameuawa na kama ikidhibitika kuwa ameuawa basi hiyo itakuwa ni hatua kubwa kwa Marekani na Pakistan ktk harakati zao za kuliangamiza kundi la Taliban pamoja na al-Qaeda.Mehsud ndiye anayeshukiwa kuongoza mashambulizi yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan Bi.Benazir Bhutto.

No comments:

Post a Comment