Thursday, December 31, 2009

Exodus

Nawatakia Nyote Heri Ya Mwaka Mpya 2010 hasa kwa wale wapenzi wa reggae tuanze mwaka mpya kwa Amani na Mafanikio.PEACE & LOVE

Friday, December 4, 2009

Ozone-Layer inavyoonekana yenye rangi ya blue na jua kwa mbali ambapo picha hii imepigwa na wana-anga kutoka ktk kituo cha kimataifa cha anga kinachoelea angani.

Thursday, October 8, 2009

Queen Ifrica



Mwanamama Queen Ifrica anatarajia kuzindua album yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina 'Montego Bay' iliyorekodiwa ktk studio za Vp Records.Aakielezea kuhusu ujio wa album hiyo alisema itasheheni takribani nyimbo 13 zitakazobeba ujumbe wa aina tofauti kama vile kiriho,burudani pamaoja na za mahusiano ya kimapenzi.Baadhi ya nyibo zilizo ktk album hiyo ni pamoja na Lioness On The Rise,Keep It To Yourself,Calling Africa,Daddy na nyinginezo nyingi..Usiikose

Tuesday, August 25, 2009

SEOUL

Seoul ni jiji linapatikana nchini Korea Kusini na ndilo jiji linaloshika nafasi ya kwanza kwa ukubwa duniani likiwa na idadi kubwa kabisa ya wakazi 10,231,000.

Sao Paolo

Sao Paolo linashika nafasi ya pili kwa ukubwa duniani likiwa na idadi ya wakazi 10,009,000 na linapatikana nchini Brazil.

Monday, August 24, 2009

Bombay

Ni jiji la tatu duniani kwa ukubwa linalopatikana nchin India likiwa na idadi ya watu 9,927,000.

Saturday, August 22, 2009

One Love

Si vibaya leo tukijikumbusha One Love kutoka kwa muasisi wa reggae Duniani hayati
Robert Nesta Marley.Pata burudani na ujumbe....

Saturday, August 15, 2009

ROKETI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI


Leo nimewaletea picha ya roketi kubwa kuliko zote duniani(Ares I-X) inayotengenezwa na wanasayansi wa Marekani ikiwa ktk hatua za mwisho kabisa za matengenezo kabla ya kuanza safari yake.Roketi hiyo yenye urefu wa ft.327 inatarajiwa kuanza safari yake baadaye mwaka huu ikiwa na lengo la kufanikisha safari ya pili ya Marekani kufika mwezini baada ya ile ya miaka ya sitini.

Friday, August 14, 2009

KIREFU CHA JINA LA MJI - MOSHI

Wachaga wenzangu je kirefu cha MOSHI mnakijua; kama hamkijui ni hiki
> hapa:-
>
> kirefu cha mji wa MOSHI
>
> M – Mungu
> O- Onyesha
> S- Sasa
> H- Hela
> I – Ilipo
>
> Wachaga oyee eeeee!!!!!!1

USINYWE RED BULL -- NI HATARI KWA MAISHA YAKO – HASA VIJANA


RED BULL Huuzwa  katika maduka makubwa (Supermarkets) na madogo (Retail
Shops) katika nchi ya Tanzania na watu wazima na watoto wetu wengi wana
mazoea ya kunywa kinywaji hiki ambacho kinaweza kusababisha kifo!

Kemikali zinazopatikana katika kinywaji cha RED BULL zilitengenezwa maalum
katika maabara za kijeshi za Ma rekani kwa ajili ya kutuliza mzuka wa
maaskari wao wakati wakitekeleza mauaji ya kikatili sana dhidi ya
wananchi wa Vietnam miaka ya sitini na sabini. Kemikali hizo zilitumika
pia kama dawa ya kuwazindua watu waliozirai (“stress coma”).
Hazikukusudiwa kutumiwa kama kinywaji au kilevi cha kawaida!

Duniani kinywaji hiki (RED BULL) huuzwa kama kitu cha kuleta msismko
(Energizer Drink) na matangazo yake yanataja sifa zake kama ifwatavyo.

“Ni kinywaji kinachompa mtu nguvu ya kustahimili na umakini. Humpa mtu
kasi ya vitendo” ... na kadhalika.

RED BULL imesambaa katika nchi 100 kwa mpigo (nchi masikini!). Na
matangazo yake kuwalenga vijana na watoto, hasa wanamichezo. Hawa ni
rahisi kushabikia kinywaji hiki kibaya na kudhurika kiafya baadaye.

Katika hali yake ya matumizi ya sasa kinywaji hiki kiligunduliwa na
Mjerumani Dietrich Mateschitz ambaye alikikuta huko Hong Kong kikiwa ni
mojawapo ya madawa yaliyotumika katika kutengeneza dawa ya mswaki wa
meno.

Dawa hiyo ilitengenezwa kwa kemikali ambazo zina kafeni na taurini
(“caffeine and “taurine). Mjerumani huyo aliona vijana wajinga wa huko
wakishabikia unywaji wake akaona mwanya wa kufanya biashara na akafanikiwa
kukileta ulaya.

ATHARI ZA KUNYWA RED BULL

Kinywaji kinachotengenezwa na kusambazwa leo hivi kina kemikali mbaya
iitwayo “Glucuronolactone”, kemikali hatari ambayo ilitengenezwa na idara
ya jeshi la Marekani wakati wa vita na Vietnam kwa ajili ya kutuliza
mvurugiko wa mwazo wa maaskari wake uliotokana na mauaji ya kinyama
waliokuwa wanafanya huko Vietnam.

Kwa sababu ya madhara makubwa ya kinywaji hiki nchi za FRANCE na DENMARK
zimepiga marufuku kinywaji hiki na kibatiza jina la “MKOROGO WA UMAUTI”.
Katika nchi hizi, utafiti uligundua kuwa maaskari wa Marekani waliotumia
kinywaji chenye kemikali ya “GLUCURONOLACTONE” waliishia kupata madhara ya
maumivu makali ya kichwa, uvimbe wa ubongo na hata ugonjwa wa ini
(Migraines, Cerebral tumours and liver diseases). Ni kwa sababu hiyo
wamarekani waliacha kuwapa maaskari wao hicho kinywaji katika miaka ya
sitini na sabini.

Jambo la kushangaza ni kuwa lebo ya RED BULL inaonyesha wazi kuwa kinwaji
hiki kimetengenezwa kwa kemikali hatari ya “GLUCURONOLACTONE”! Ni kwa
sababu hiyo serikali za Denmark na Ufaransa nazo zikapiga marufuku unywaji
wa RED BULL.

Pamoja na wauzaji wa RED BULL kuweka bayana kuwa ndani mwake mna hiyo
kemikali hatari ya “GLUCURONOLACTONE” lebo ya RED BULL hailezi madhara
makubwa yanayoletwa na kemikali hiyo. Madhara ambayo hayakuwekwa bayana
kwa mnywaji ni kama yafuatayo:

1.Ni hatari kwa mtu ambaye hafanyi kazi au mazoezi mazito sana kukitumia
kwani kina tabia ya kuongeza msukumo wa damu na kasi ya mapigo ya moyo
kiasi kwamba mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa moyo.
2.Mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa damu kuvuja ubongoni kwani RED
BULL ina kemikali zinazoifanya damu iwe nyembaba ili moyo upate kusukuma
damu nyingi bila kutumia nguvu nyingi.
3.Ni hatari kuchanganya RED BULL na pombe ya aina yoyote kwani
mchanganyiko wake huwa ni sumu (“Deadly Bomb”) inayoathiri musuli za ini
la mtumiaji na kuiacha katika hali ambayo haitapona kamwe.
4.RED BULL Ina vitamini B12 kwa wingi, vitamini ambayo hutumiwa kama dawa
ya kuwazindua wagonjwa mahututi. Matumizi ya vitamini hii katika watu
wazima ina athari za kuleta shinikizo la damu na humfanya mtu ajisikie
kama mlevi.
5.Unywaji wa RED BULL mara kwa mara huvuruga mfumo ya neva za fahamu na
husababisha maradhi mithili ya mfadhaiko wa akili usioponyeka.

HITIMISHO::
RED BULL ni kinywaji HATARI SANA ambacho hapana budi kipigwe marufuku
katika nchi zote zinazoendelea kwani ni dhahiri kimetengenezwa na
kusambazwa ili kiathiri afya za wananchi wasiojiweza wa nchi hizi
masikini. Kwa kuwa wengi katika nchi hizi hutumia pombe za kila aina ni
wazi kuwa kinywaji hiki kinalenga kuwamaliza watu wetu – kana kwamba
ukimwi uliobuniwa na hao wabaya wetu hautoshi! N I VYEMA TUKAWALINDA
WATOTO NA VIJANA WETU LA SIVYO HATUNA WARITHI!

Tafsiri – EGM 2009

Thursday, August 13, 2009

Product Mpya Kutoka Microsoft


Kampuni ya kutengeneza Computer na Software ya Microsot imezindua Computer mpya ijulikanayo kama Surface Computer ambayo itatumika zaidi katika Hoteli,Restaurants,Maduka ya rejareja pamoja na Casino.Computer hiyo iliyo ktk muundo wa meza yenye upana wa inch 30 itakupa uwezo wa kuitumia kama meza na wakati huo huo kama computer ambapo itakupa uwezo wa ku-browse miji mbalimbali, kutoa oda na hata kusikiliza au ku-download miziki au picha mbalimbali ktk internet.

Tuesday, August 11, 2009

Computer hiyo ina uwezo wa kutambua vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi pamoja na digital kamera.Unapoiweka simu yako kwenye kioo cha computer hiyo huitambua ni aina gani,uwezo wake na pia unaweza ku-update picha pamoja na milio mbalimbali ya simu yako kama inavyoonekana kwenye picha.
Hili ni gari maalum la kubeba wafanyakazi wa kampuni ya Microsoft Co. ambapo wafakazi hupata fursa ya kuendelea na kazi wawapo njiani kuelekea kazini kuokoa muda unaopotea kutokana na msongamano wa magari.

Zana Mpya Za Kivita

Dege jipya la kivita la Marekani aina F-16D lililotengenezwa kwa teknologia ijulikanayo kama ACAT(Automatic Collision Avoidance Technology ) likiruka kutoka ktk uwanja wa Edward Air Force Base huko Florida.Dege hili jipya la kivita lina uwezo wa kuzuia mashambulizi lenyewe au automatic kama wazungu wanavyosema likiwa ardhini au angani.

Monday, August 10, 2009

Kilio Cha Mtu Mzima

Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo.Mfululizo wamabomu ya kutegwa ardhini pamoja na yale ya kujitoa mhanga umesababisha vifo vya watu takriban 42 nchini Iraq na kujeruhi wengine zaidi ya 100.Hali hiyo nchini Iraq sasa imekuwa ni kitu cha kawaida ambapo kwa siku watu kadhaa hufa kutokana na mapigano ya hapa na pale yanayotokana na makundi mbalimbali yaliyokuwepo na yaliyoibuka baada ya vita iliyoongozwa na Marekani kumalizika.HEBU TAZAMA MTU MZIMA HUYU ANAVYOLIA...........!!!

Typhoon Yazidi Kuwa Tishio


Upepo mkali unaoambatana na mvua (Typhoon) uliyokikumba kisiwa cha Taiwan siku chache zilizopita sasa umeingia mashariki mwa china kwa kasi ya km 84 kwa saa.upepo huo uliyoleta maafa makubwa nchini Taiwani umeshaaribu mashamba mengi ya wakulima nchini China pamoja na kuharibu miundo mbinu.Serekali ya China mpaka kufikia sasa imekwisha waamisha watu zaidi ya milioni moja mashariki mwa nchi hiyo ili kuweza kupunguza maafa yanayotokana na upepo huo.

ISLAMABAD


Uchunguzi uliyofanyika hivi karibuni nchini Pakistan unaonyesha kuwa 59% ya wananchi wamechoshwa vitendo pamoja na majeshi ya Marekani kuwepo katika nchi yao.Wakitoa maoni yao kutoka maeneo mbali mabli yanchi hiyo wanachi hao walisema vita,njaa pamoja na vitendo vya kujitoa mhanga vinavyotokea mara kwa mara havisababishwi na ndugu zao India kama ambavyo wengi walivyokuwa wadhani bali yanatokana na siasa za kimarekani ndani ya nchi yao na wametaka siasa hizo zikome na wamarekani hao waondoke haraka iwezekanavyo ktk ardhi yao.

Friday, August 7, 2009

Marekani Kutoa Msaada Wa Kijeshi Kwa Somalia


Marekani imeahidi Kuendelea kutoa msaada wa kijeshi kwa Somalia ili kuisaidia ili kuweza kuisadia serekali kupambana na wapiganaji wa kiislam.Akitoa ahadi kwa rais wa Somalia yaliyofanyika jana jijini Nairobi waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton alisema rais Obama na serikali yake wako tayari kutoa misaada mbalimbali serekali hiyo kufikia malengo yake ya kuingoza nchi nzima.Nchi ya Somalia kwa karibu miongo miwili sasa imekosa serekali imara baada ya kuibuka makundi mbalimbali ya kivita yakipambana huku kila kundi likitaka kuongoza nchi lakini kwa hivi sasa kundi kubwa la Kiislam la al-Shabab ndilo linaloonekana kuwa na nguvu zaidi baada ya kuwa limeshikilia sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia.

PAKISTAN


Maafisa usalama wa Marekani pamoja na Pakistan wamesema huenda kiongozi wa Taliban nchini Pakistan ambaye alikuwa akiongoza mashambulizi ya kujitoa mhanga dhidi ya serikali ya Pakistan Chief Baitullah Mehsud ameuawa ktk mashambulizi ya roketi yaliyofanywa na kikosi cha CIA.Habari zinazidi kusema kwamba katika mashambulizi hayo yaliyofanywa na CIA dhidi ya vikosi vya Taliban huenda Mehsud ameuawa na kama ikidhibitika kuwa ameuawa basi hiyo itakuwa ni hatua kubwa kwa Marekani na Pakistan ktk harakati zao za kuliangamiza kundi la Taliban pamoja na al-Qaeda.Mehsud ndiye anayeshukiwa kuongoza mashambulizi yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan Bi.Benazir Bhutto.

Thursday, August 6, 2009

Uhaba Mkubwa Wa Maji Nchini Somalia


Uhaba mkubwa wa maji umeikumba Somalia na kusababisha hali kuwa mbaya zaidi kwa wananchi pamoja na mifugo.Hali inazidi kuwa mbaya zaidi hata kufikia watu kushindwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutafuta maji kutokana na hali ya udhoofu inayowakabili wananchi pamoja na mifugo yao,chanzo cha habari kilieleza.Mifereji ya maji na mito vimekauka,mifugo na binadamu wanakufa na hali inazidi kuwa mbaya siku kwa siku nchini Somali kwa hakika ndugu zetu wanateseka.